Mgogoro wa mpaka kati ya Vijiji viwili vya Chigwingwili Kata ya Mtanana na Hogoro Kata ya Hogoro uliodumu tangu kugawanywa kwa Wilaya za Mpwapwa na Kongwa 1995 sasa kupatiwa ufumbuzi.
Akijibu maswali ya wananchi wa Kata ya Mtanana katika mkutano wa hadhara, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mheshimiwa Mayeka Simon amemtaka Afisa ardhi Wilaya kuandaa nyaraka zote zilizotumika kutatua mgogoro huo tangu awali ili awaite viongozi wa Vijiji hivyo na kupima upya kwa dhumuni la kutatua swala la mgogoro wa mpaka huo.
Akifafanua hali ya mgoro huo Afisa ardhi Wilaya ya Kongwa Bwana Meshack Mlaponi amesema kuwa Mwaka 2023 ofisi ya ardhi Wilaya ya Kongwa ilipima na kuweka alama kwenye mpaka lakini uongozi wa Kijiji cha Hogoro wamekuwa wakiendelea kuukataa mpaka huo kwakuwa GPS ilionesha kuwa eneo ambalo huwa wanatumia kwaajili ya mashamba liliangukia Kijiji cha Chigwingwili.
Vilevile Mheshimiwa Mayeka amepata wasaa wa kujibu hoja nyingine za wananchi ikiwemo swala la Kituo cha Afya na kueleza kuwa Kata ya Mtanana ina hadhi na sifa ya kuwa na kituo cha afya hivyo amewaahidi wananchi hao kupatiwa kituo cha afya na pia wananchi wa Kijiji cha Ndalibo watapatiwa Zahanati ili waweze kupata huduma za afya Ndani ya kijiji Chao.
Pia Mheshimiwa Mayeka ametumia hadhara hiyo kuwaambia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya Sita imeleta fedha za kusambaza umeme maeneo yote yaliyobaki katika Wilaya ya Kongwa na kituo cha umeme kitajengwa katika Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni hivyo upatikanaji wa nishati ya umeme utakuwa wa uhakika.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.