Na Stephen Jackson, Kongwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwaa meitaka Taliri na Wizara ya Mifugo kuweka mazingira rafiki katika Kituo Atamizi cha Ufugaji wa kibiashara kwa Vijana kilichopo eneo la Mbande Kata ya Sejeli ili kuwezesha Vijana wengi kufanya biashara ikiwemo nyama choma.
Mhe. Majaliwa amesema Wizara ya Mifugo na uvuvi, Taliri kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ni vema wakaweka Miundombinu itakayowawezesha Vijana wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali kupitia uchomaji nyama Kijiji cha Mbande na maeneo mengine kuhamishia shughuli zao katika Kituo cha Taliri Kilichopo eneo la Mbande Kata ya Sejeli.
Mhe. Majaliwa alisema hayo wakati akihutubia Wananchi kwenye hafla ya makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Ufugaji wa kibiashara kwa Vijana - Kongwa kati ya "Private Agricultural Sector Support" (PASS) na Kituo cha utafiti wa mifugo Taliri.
Mhe. Majaliwa alisisitiza Wizara ya Mifugo na uvuvi kufanya kazi kwa ukaribu na uongozi wa Halmashauri ili kukuza ufanisi wa Kituo hicho kwani Wakuu wa Divisheni na Vitengo hususani Seksheni ya Mifugo na maendeleo ya Jamii kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu.
Mhe. Majaliwa alitutumia fursa hiyo kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika kwenye maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura sanjari na kushiriki kutoa maoni yao katika maandalizi ya dira ya maendeleo ya taifa 2050.
Akihitimisha hotuba yake Mhe. Majaliwa, aliipongeza Wizara ya Mifugo na uvuvi, PASS na Taliri kwa kufanikisha kukamilika kwa Kituo hicho.
Kwa upande wake Mhe. Abdala Ulega, Waziri wa Mifugo na Uvuvi aliutaarifu umma kuwa nyama ya mbuzi inapendwa kwa asilimia 70% ikilinganishwa na nyama nyingine huku nyingi ikitoka mkoani Dodoma.
"Nyama ya mbuzi inayoongoza kwa kuoendwa ni Ile inayotoka katika mkoa wa Dodoma"
"Kituo kikubwa cha nyama ya mbuzi hapa nchini kitakuwa ni hapa Kongwa" Abdallah Ulega Waziri wa mifugo na uvuvi.
Katika Hafla hiyo viongozi mbalimbali walizungumza na Wananchi akiwemo Mhe. Rosemary Senyamule Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
ambaye alisema katika kipindi cha miaka mitatu Mkoa wa Dodoma umepata miradi mikubwa kama vile ujenzi wa majosho 59, mizani 13 inayotumika minadani, ukarabati wa machinjio manne, minada miwili imewekwa uzio, pikipiki 45 za wataalamu wa mifugo, dawa za kuogeshea mifugo, Mifugo 332,000 ilipatiwa chanjo, ujenzi wa malambo manne ya maji na ujenzi wa mabwawa mawili katika Wilaya za Kongwa na Chamwino unaendelea. Aidha Senyamule ameeleza kuwa Mkoa umefanikiwa kutatua baadhi ya migogoro ya wakulima na wafugaji ilitodumu kwa muda mrefu.
Mhe. Job Ndugai Spika Mstaafu na mbunge wa Jimbo la Kongwa aliyeshauri Vijana waanzilishi wa Kituo hicho cha unenepeshaji mbuzi wapewe Mbuzi kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kupitia Ufugaji waliokifunza kupitia Kituo hicho, Jambo lililoungwa mkono na Waziri wa mifugo kwamba Jumla ya mbuzi 60 watatolewa kwa Vijana hao.
Akizungumza kwa niaba ya bodi ya wakurugenzi wa PASS, Bwana Charse Chenza Mwenyekiti wa bodi hiyo alisema, Pamoja na mambo mengine, PASS ipo kuwezesha Wananchi, vikundi makampuni au wakulima wasio na dhamana ya kukopesheka benki, hivyo jukumu la PASS ni kuwawekea dhamana.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.