Na Stephen Jackson
Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mbunge wa jimbo la uchaguzi la Kongwa Mhe. Jobu Y. Ndugai amewataka viongozi wa chama na serikali kuwa mfano kwenye ushiriki wa shughuli za miradi mbalimbali ya maendeleo zinazotekelezwa na wananchi.
Mhe. Ndugai amesema hayo wakati akizungumza na baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa lililoketi tarehe 19 Agosti 2021 kujadili taarifa ya robo ya nne ya mwaka wa Fedha 2020/2021 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri. ‘’Inchi hii imekuwa ya ukaguzi anayejenga nani?’’ Amesema Mheshimiwa Ndugai.
Aidha Mhe. Ndugai ametoa rai kwa viongozi wote nchini kushiriki pamoja na wananchi kwenye utekelezaji wa shughuli mbalimbali badala ya kusubiri kufanya ukaguzi, kauli ambayo imeungwa mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM (W) Mwl. Mussa Abdi Matari. ‘’Nadhani alichosema ni cha maana sana ndo maana huwa hanioni ninaenda kukagua,’’ Lakini viongozi siku hizi imekuwa kazi ya maneno tu’’ Alisema Mussa Abdi Matari.
Mheshimiwa Ndugai ametumia fursa hiyo pia kuwaagiza madiwani wote wa Halmashauri ya Kongwa kuwahamasisha wanafunzi wa darasa la saba kufanya vizuri katika mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi unaotarajiwa kufanyika Mwezi ujao ili kuepuka rekodi mbaya ya ufaulu.
Kuhusu suala la chanjo, Mhe. Ndugai amewaasa viongozi na wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo kwa kuwa ni muhimu kwa afya na maendeleo ya wanachi.
Naye mkuu wa wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel amewataka viongozi kuzingatia kauli ya Mheshimiwa Spika kwa kushiriki kiamilifu katika kufanya shughuli mbalimbali ili kuwa sehemu ya ufanisi wa miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.
Mkutano huo wa baraza umehudhuriwa na wajumbe wa baraza hilo wakiwemo wenyeviti wa mabaraza ya Mamlaka za miji midogo ya Kongwa na Kibaigwa na Baadhi ya wataalamu kutoka taasisi mbalimbali.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.