Jumla ya miradi 6 yenye thamani ya Tsh. 3,131,091,240/= imepitiwa na Mwenge wa Uhuru Wilayani Kongwa, ambapo Halmashauri ya Wilaya imechangia Tsh. 794,000/= , Wahisani Tsh. 169,007,740/= , Serikali Kuu Tsh. 428,500,000/= , Wananchi Tsh. 23,989,500/= na Sekta Binafsi Tsh. 2,508,800,000/=.
MKatika Mbio hizo kulifanyika uzinduzi, ufunguzi na uwekaji wa mawe ya msing katika maeneo mbalimbali ya miradi kama ifuatavyo; Kibaigwa - Uzinduzi wa Soko la Mbogamboga na Matunda Kibaigwa wenye thamani ya shilingi 166,825,240/= ambao umefadhiliwa na Mradi wa Uboreshaji wa Mazingira ya Biasha (LIC Project) na Kuweka Jiwe la Msingi ujenzi wa kiwanda cha kukamua Mafuta ya Alizeti (Kahama Oil Mill) – mradi uliogharimu shilingi 2,500,000,000/= na ni sekta binafsi; Ibwaga - Ufunguzi wa Mabweni katika Shule ya Sekondari Ibwaga yenye thamani ya shilingi 150,000,000/= , mradi huu umetekelezwa kupiti fedha za mpango wa malipo kwa matokeo (P4R); Mtanana - Uzinduzi wa Mradiwa Maji katika Kijiji cha Chigwingwili, mradi wenye thanai ya shilingi 253,500,000/= katika fedha hizo wananchi wamechangia Tsh 5,000,000 na zilizosalia zimetoka Serikali Kuu; Mkoka - Uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mkoka, na Uwekaji wa Jiwe la Msingi, ujenzi wa jengo la huduma ya upasuaji katika Kituo cha Afya Mkoka.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.