Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Nchini Tanzania Bi. Sarah Gordon-Gibson ametembelea soko la mahindi la kimataifa Kibaigwa Julai 5, 2023 kwa nia ya kujionea hali halisi ya utendaji kazi wa soko hilo.
Katika ziara yake Bi. Sarah amezungumza na wafanyabiashara sokoni hapo na pia kujionea hali halisi ya uendeshwaji wa soko.
Akihitimisha ziara yake amewashukuru wananchi na Viongozi waliojitokeza kwenye ziara hiyo na ameahidi kuwa atarejea rasmi wakati mwingine kwa ajili ya kutathmini jinsi ofisi yake inavyoweza kuchangia maboresho ya soko hilo.
Kufuatia ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel, amemshukuru kiongozi huyo kwa kufanya ziara hiyo katika Soko hilo.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.