Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt Omary Nkullo amekabidhi pikipiki mbili kwa maafisa afya wa Tarafa za Kongwa na Zoissa kwaajili ya kusaidia usimamizi na ukaguzi wa shughuli mbalimbali ikiwemo ukaguzi wa usafi wa mazingira kwenye maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kongwa.
Akikabidhi pikipiki hizo katika viunga vya Halmashauri, Dkt Omary Nkullo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Afya inayosimamia mradi wa maji na usafi wa mazingira vijijini (SRWSS) kwa kuwezesha usambazwaji wa pikipiki hizo ambazo zitakwenda kuongeza kasi ya ukaguzi wa Mazingira.
Aidha Dkt Nkullo amewasihi maafisa afya hao kuzitunza na kutumia pikipiki hizo kutimiza lengo lililokusudiwa ili ziongeze kasi na zirahisishe zoezi la ukaguzi wa Mazingira na kuhakikisha kuwa maeneo mbalimbali kama vile migahawa na sehemu nyingine zinazotumiwa kwa wingi na wananchi kunakuwa na vyoo bora na wananchi wanapatiwa elimu juu ya usafi wa mazingira.
Ma-afisa afya waliokabidhiwa pikipiki hizo wametoa shukrani zao za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na kuahidi kutekeleza malengo ya Wizara ya Afya inayosimamia mradi wa maji na usafi wa mazingira vijijini (SRWSS).
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.