Na. Bernadethat Mwakilabi,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kongwa Dkt Omary Nkullo amewataka wanafunzi wa darasa la saba kuweka juhudi na jitihada za kufanya vizuri katika mitihani yao ya Taifa ili waweze kufaulu na kuendelea na masomo ya sekondari.
Dkt. Omary Nkullo ameyasema hayo akiwa shule ya msingi Mbande alipokwenda kwaajili ya kushiriki chakula cha pamoja na wanafunzi hao 177 wanaotarajia kufanya mtihani wao wa Taifa septemba 11-12 mwaka huu shuleni hapo.
Aidha Dkt. Omary Nkullo amewataka wanafunzi hao kukataa kabisa suala la kufanyishwa kazi za ndani muda ambao wanatakiwa wasome ili kujiandaa vyema na mitihani kwani Serikali ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan imeweka nguvu kubwa kwenye sekta ya elimu ikiwemo kujenga madarasa na kusomesha wanafunzi bure ili kupata matokeo chanya ikiwemo wanafunzi wengi zaidi kupata fursa hiyo ya elimu.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Sejeli Mhe. Chilingo Chimeledya licha ya kukiri ushirikiano baina ya Serikali ya Kijiji na Wananchi lakini pia ameshukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha miundombinu ya elimu katika Kata hiyo.
Nae Afisa Elimu Msingi (taaluma) ndugu Juma Butiye amewasihi walimu kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kuishi na jamii katika kipindi ambacho watakuwa wamemaliza masomo.
Katika hafla hiyo pia yamefanyika maombi ya pamoja kwa ajili ya kuwaombea wanafunzi wote 8,160 wa Darasa la saba wilayani Kongwa wanaotarajia kufanya mtihani wao wa Taifa mwaka huu.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.