Na Stephen Jackson - Kongwa DC
Mkuu mpya wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remedius Mwema Emmanuel ameahidi kufanya kazi kwa Ushirikiano, Utii na Uadilifu katika kipindi chake cha uongozi.
Mhe. Emmanuel, amesema hayo baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo wa ukuu wa wilaya ya Kongwa. Kiapo hicho kimetolewa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, ambaye amewaasa wakuu hao wapya wa wilaya, kutokuwa na ulimbukeni wa madaraka na hivyo wafanye kazi zenye matokeo chanya.
Kwa upande mwingine Mkuu wa wilaya ya Kongwa, ametumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua kuwa miongoni mwa vijana wachache wanaomsaidia.
Hivyo basi kwa namna ya pekee ameahidi pia kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuwaletea maendeleo wananchi, hususani wa Wilaya ya Kongwa. Mhe. Remedius Mwema Emanuel anachukua nafasi ya Mheshimiwa Dr. Suleimani Serera ambaye amebadilishwa kituo cha kazi.
Hafla hiyo ya kuapishwa Wakuu wa Wilaya za Kongwa na Kondoa imefanyika leo Juni 22, mwaka 2021 Mkoani Dodoma ambapo Wakuu wa Wilaya mbili wameapishwa akiwemo Dr. Dk Khamis Mkanachi aliyeapishwa kushika wadhifa huo Wilayani Kondoa.
Miongoni mwa wageni waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Wakuu wa Wilaya nyingine za mkoa wa Dodoma, wakiwemo wale waliobadilishwa vituo vya kazi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.