Na. Mbonea E. Masha
Mkuu wa gereza Kongwa Sp. Tekla Erasto Ngilangwa amepewa zawadi ya pongezi na Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya Kongwa kwa kazi nzuri ambayo ameendelea kufanya toka alipoanza kazi katika nafasi hiyo.
Akimkabidhi zawadi hiyo, mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kongwa amesema anafahamu hali ya gereza Kongwa ilivyokuwa kipindi Sp Tekla Erasto anachukuwa nafasi kama mkuu wa gereza na jitihada na hatua zilizochukuliwa kubadilisha mazingira na kuboresha hali ya gereza ni jitihada kubwa zinazohitaji pongezi sana. Ameongeza kuwa kuna utofauti mkubwa kipindi Sp Tekla Erasto anaanza kazi yake kama mkuu wa gereza na hivi sasa, maboresho yaliyofanyika ni makubwa na kazi nzuri imefanyika na inaendelea kufanyika.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi, Sp. Tekla Erasto ametoa shukrani zake za dhati kwa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya Kongwa kwa kuona mchango wake na juhudi zake na kuahidi kuendelea kufanya kazi kubwa ili hata waliomuamini kwa nafasi hiyo wafurahi kwa uamuzi huo na pia iwe ni chachu kwa wanawake wengi zaidi kuaminika katika nafasi hiyo ya ukuu wa gereza.
Zoezi la utoaji zawadi limefanyika katika Ukumbi wa chama cha mapinduzi wilayani Kongwa katika mkutano wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi kujadili taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.