MKUU WA JESHI LA NCHI KAVU WA NAMIBIA AFANYA ZIARA WILAYANI KONGWA
Habari Kongwa DC
Mkuu wa Jeshi la N chi kavuwa Namibia amefanya ziara Wilayani Kongwa kwa dhumuni la kutembelea kambi ya wapigania uhuru ikiwemo eneo aliloishi baba wa Taifa la Namibia Hayati Sam Nujoma na kupokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka S Mayeka.
Mhe. Mayeka ameonesha kufurahishwa kwake kwa ugeni huo na kueleza kuwa ziara hiyo ni muhimu kujenga uelewa wa uwepo wa maeneo haya yaliyotumiwa na Nchi tano kupigania uhuru wa Nchi zao na kuongeza kuwa ni jukumu la nchi zote kudumisha undugu na historia adhimu uli vizazi vijavyo vitambue historia ya nchi hizi mbili na namna zilivypokuwa na mshikamano katika mapambano ya uhuru.
Baadhi ya maeneo aliyotembelea ni pamoja na ofisi zilizotumiwa na wapigania uhuru, nyumba walizoishi wapigania uhuru, maeneo yaliyotumiwa na wapigania uhuru kujifunza mbinu za kijeshi, makaburi ambapo miili ya wapigania uhuru ilihifadhiwa pamoja na uwanja wa ndege uliotumiwa na wapigania uhuru.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.