Na Stephen Jackson
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel, amepongeza jitihada za viongozi na Wananchi wote wa Kongwa waliojitokeza kumuunga mkono katika zoezi la kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali.
Pongezi hizo zimetolewa na kiongozi huyo baada ya zoezi kukamilika kwa ufanisi, ambapo yeye binafsi ameshirikiana na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kufanya usafi katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Kibaigwa.
Maeneo yaliyofanyiwa usafi ni Kibaigwa, Mbande, VETA, Shule ya Sekondari Sejeli, Hospitali ya Wilaya, Viwanja utakapofanyika Mkesha wa Mwenge na eneo la Mradi wa maji wa Ibwaga.
Kufuatia mwitikio huo chanya, Mhe. Mwema ametoa wito kwa kwa Viongozi na Wananchi kudumisha utamaduni wa kufanya usafi wa Mazingira kila Mara pasipo kusukumwa ili Kujenga Kongwa yenye mafanikio.
"Nimefarijika kuiona Kongwa yenye juhudi pale tunapokubaliana katika jambo fulani lenye tija kwa ustawi wa Wilaya yetu". Kauli ya DC Mwema.
Miongoni mwa wadau walioshiriki zoezi ni Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji (W), Wakuu wa Taasisi Mbalimbali, Wakuu wa Idara, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Waheshimiwa Madiwani, Maafisa Tarafa, Viongozi wa Madhehebu ya dini, Watumishi na baadhi ya Wananchi.
Aidha Mhe. Mwema amesisitiza Wananchi kuendelea kuchukua Tahadhari dhidi ya ugonjwa wa "Corona'' wakati wanapofanya maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru Julai 30 Mwezi huu.
Zoezi la usafi wa Mazingira limefanyika kufuatia agizo la Mkuu wa Wilaya alilolitoa hivi karibuni kuwa shughuli hiyo ifanyike siku ya Jumamosi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.