Na Stephen Jackson, Kongwa.
Wananchi wilayani Kongwa wamehamasika na utolewaji wa chanjo ya Polio inayotolewa nchi nzima kupitia uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika Agosti 2, 2022 ngazi ya Wilaya katika Kijiji cha Makawa.
Akizungumza na Wananchi wa Kijiji Cha Makawa, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel amesema Serikali imetoa fedha ili kuwakinga watanzania na ugonjwa wa Polio ili kuwawezesha wananchi kutimiza maono yao.
Aidha amesisitiza kuwa lengo la jumla la Wilaya ya Kongwa ni kuwa ya kwanza katika utekelezaji wa sera na Maagizo ya Serikali.
Katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya amezindua kampeni ya Utoaji chanjo hiyo Kwa ngazi ya Wilaya inayotarajiwa kudumu Kwa siku nne ikianzia Septemba mosi, 2022.
Dkt. Fransis Lutalala kutoka Ofisi ya Afya Mkoa wa Dodoma anayesimamia zoezi Wilaya ya Kongwa amesema kuwa Mkoa umejipanga kuwapatia chanjo hiyo watoto wote wanaostahili ili waweze kuvuka lengo ambapo Kwa siku ya kwanza ya kampeni jumla ya watoto 30,000 sawa na 32% ya lengo.
Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Thomas Samwel ametoa elimu juu ya chimbuko la ugonjwa huu Kwa siku za karibuni na kuwaasa wananchi kuchukua hatua Kwa kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha watoto wanapata chanjo.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.