Na Stephen Jackson, Kongwa DC
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka, amepiga marufuku walimu kujimilikisha mashamba ya shule, ili mashamba hayo yatumike kuzalisha chakula cha Wanafunzi.
Maelekezo hayo yametolewa katika kikao cha Tathmini ya hali ya Lishe Wilaya ya Kongwa, Kilichofanyika ukumbi wa Hospitali ya Wilaya Januari 23, 2024.
Sambamba na Agizo hilo Mhe. Mayeka, ameelekeza Watendaji wa Vijiji na kata kuwasaka nyumba kwa nyumba wanafunzi wote ambao hawajaripoti shuleni tangu shule zilipofunguliwa mapema mwezi huu.
" Muwasake nyumba kwa nyumba ili waendelee na masomo" Alinukuliwa Mhe. Mayeka.
Akiwasilisha taarifa ya hali ya Lishe, Afisa Lishe Wilaya ya Kongwa Bi. Maria Haule alisema Asilimia 75.5% ya wanafunzi wilayani Kongwa wanapata chakula shuleni ambapo kata za Chitego, Zoissa na Ugogoni zinaogoza kwa utoaji chakula kwa 100% huku kata ya chiwe ikishika nafasi ya Mwisho kwa asilimia 38.95%
Aidha Bi. Haule alitaja kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa RTK kwa ajili ya upimaji wa madini joto kwenye chakula na idadi ndogo ya wanafunzi wanaopata chakula shuleni ambapo kati ya wanafunzi 123,390 wanafunzi.93,291 ndio wanaopata chakula, huku watoto wapatao 43 wakiibuliwa katika jamii na kupatiwa matibabu ya utapiamlo.
Kikao Cha tathmini ya hali ya lishe kimehusisha wadau wa Lishe Wilaya ya Kongwa wakiwemo CUAMM, na World Vision ambao nao walipata fursa ya kuwasilisha taarifa zao.
Bi. Flora Manyanda Mdau (CUAMM) alisema shirika lake limekuwa likiwezesha upatikanaji wa chakula dawa, pamoja na viambaupishi kwa siku za Afya na lishe, ingawa ametaja kuwepo kwa mahudhurio hafifu ya wananchi hususani jamii ya Wanaume.
Naye Bwana Simon Kutamika (World Vision) alieleza wajumbe wa kikao kuwa Shirika la Word Vision lipo mbioni kutoa matokeo ya Tathmini ya hali ya lishe iliyofanywa katika vijiji 10 ndani ya kata tatu, ili kwa lengo la kuchukua hatua.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.