Na Stephen Jackson, Kongwa.
Maafisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa wameshauri wakulima wenye mashamba maeneo ya Mabondeni kuanzisha kilimo cha mpunga badala ya kuyatelekeza mashamba hayo pindi yanapojaa maji nyakati za masika.
Maafisa hao Anitha Nyerere Mathias na Josiah Chikoka walitoa ushauri huo Mei 8, 2024 walipotembelea mashamba mapya ya mpunga ya mkulima na Diwani wa kata ya Kongwa Mhe. White Zuberi Mwanzalila na Wananchi wengine yaliyopo jirani na Shule ya Sekondari Kongwa.
Kwa upande wake Bwana Chikoka alisema, Wakulima ni vema wakulima wakahamasishana kuhusu kilimo cha mpunga na kwa kuwa Halmashauri kupitia maafisa ugani itatoa ushirikiano wa kutosha.
Naye Anitha Mathias ameongeza kuwa Wakulima wakiwa wengi watasaidia kupunguza baadhi ya gharama za uendeshaji ikiwemo gharama mbalimbali kama vile kujihami ndege na wadudu waharibifu wa mazao.
Akizungumza mbele ya wataalamu hao, Mhe. White Zuberi Mwanzalila alisema, akiwa kama mkulima anashsuri wakulima wengine waliopo kwenye maeneo ya mbuga kuchangamkia fursa ya kilimo cha mpunga kwani kina tija zaidi ikilinganishwa na mazao mengine.
Mussa Mashamba Nhoni ambaye ni mkulima mzoefu wa Mpunga ameiomba Serikali kusaidia kuboresha Miundombinu ya eneo hilo ili kuepusha hasara kwa wakulima.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.