Mwenge wa uhuru 2025 umezindua klabu ya wapinga Rushwa na kutembelea mradi wa matumizi ya nishati Safi ya kupikia wenye thamani ya shilingi 20,440,800 katika chuo cha mafunzo ya stadi Veta Kongwa.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2025 Ndg Ismail Ali Ussi ameupongeza uongozi wa chuo cha Veta Kongwa kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutumia nishati safi ya kupikia na kuwataka vijana kuhamasisha matumizi hayo kwenye jamii ili kutunza mazingira.
Aidha Ndg. Ussi ameeleza kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia ni utekelezaji wa agizo la Serikali kwa taasisi zenye watu zaidi ya 100 kutumia nishati safi ya kupikia ambapo matumizi hayo yatasaidia kuokoa gharama, muda na kutunza afya.
Wakati huohuo akizindua klabu ya wapinga Rushwa chuoni hapo Ndg Ussi amewataka wanafunzi na vijana kumsaidia Mhe. Rais katika suala zima la mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa.
Mwenge wa uhuru 2025 uliobeba kauli mbiu ya “Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu.” umetembea kilomita 137.3 na kuzindua, kutembelea, kukagua kuweka mawe ya msingi na kupokea taarifa za Miradi yenye thamani ya zaidi ya billion 39.3 ikiwa ni pamoja na maabara katika shule ya sekondari Msunjilile, kliniki ya baba, mama na mtoto, nyumba moja ya walimu shule ya sekondari Manungu na ujenzi wa barabara yenye kilomita 6 kwenye bonde la mafufuriko Mtanana.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.