Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale Bi Husna Tony amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale imejifunza mengi katika ziara ya mafunzo Wilayani Kongwa na kuongeza kuwa japo Wilaya ya Nyang’wale ni wachimba madini na Kongwa ni wafugaji basi watachukua elimu waliyopata kwenye mafunzo waliyopata ili wakafanye ufugaji wenye tija watakaporudi Nyang’wale.
Bi. Husna ameeleza hayo akiwa ameongozana na Baraza la madiwani wa Wilaya ya Nyang’wale, wakuu wa Idara, Mkuu wa wilaya, Pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyang’wale katika mafunzo ya ufugaji wenye tija unaofanyika NARCO wilayani Kongwa.
Aidha, Katibu tawala Wilaya ya Nyang'wale ametoa salamu zake kwa viongozi wa Kongwa ambao ambao walipata wasaa wa kuwa wenyeji na kuambatana na msafara katika ziara, na kuongeza kuwa wamefurahia Nyama ya ngombe nzuri kutoka NARCO na kufurahia mapokezi mazuri katika Wilaya ya Kongwa.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mhe. Grace Kingalame amesema ziara hii imekuwa na tija kubwa Sana kwa viongozi wa Chama cha mapinduzi CCM madiwani, viongozi wa kata na Wilaya pamoja na wataalam wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale kwani elimu waliyoipata wataipeleka kwa wananchi wao na kuibua miradi ya maendeleo yenye dhumuni la kuinua kipato cha wananchi wa Wilaya ya Nyang’wale na kukuza Uchumi wao.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.