Wafanyakazi katika Wilaya ya Kongwa wameiomba ofisi ya utumishi kutembelea sekta zote za umma kuona idadi ya Watumishi waliopo ili kuondoa tatizo la watumishi katika Kila sekta.
Wafanyakazi hao wamesema hayo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi lililofanyoka Wilayani Kongwa ili kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi ambapo baraza limekutanisha wafanyakazi wa sekta zote za umma waliotumia kikao husika kuomba ofisi ya utumishi kuchukua hatua za kuwaajiri watumishi wanaojitolea katika sekta hizo.
Aidha wameiomba Halmashauri kuzingatia malipo ya fedha za masaa ya ziada kwa wafanyakazi wa sekta zote na kuzingatia uhamisho wenye tija na wa lazima kwa wafanyakazi.
Akisoma taarifa ya idara ya utumishi Kwa niaba ya afisa utumishi wilaya ya Kongwa Bwana Deogratius John amesema kuwa kuna swala la utoro wa watumishi utovu wa nidhamu hali iliyopelekea kusimamisha mshahara kwa watumishi nane.
Pia Bw John ameeleza mikakati iliyotolewa ili kupambana na changamoto mbalimbali za kiutumishi na kueleza kuwa ni kujitahidi kupunguza madeni ya kusafirisha mizigo ya wastaafu, kuandaa bajeti ya ajira mpya ili kuondoa upungufu wa wafanyakazi na kushughulikia utetezi wa walimu. Pia ameendelea na kutoa wito kwa vyama vya wafanyakazi kusisitiza uwajibikaji, kutekeleza majukumu yao na kuondoa chuki Kwa wafanyakazi.
Akiongea kwa niaba ya mwenyekiti wa Baraza, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bwana Fortunatus Mabula amesema kuwa anayachukua maadhimio yote yaliyotolewa katika mkutano huo na kufikisha katika ofisi ya Mkurugenzi kwani hoja hizo ni muhimu Kwa ustawi wa sekta zote.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.