Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deogratius Ndejembi azindua rasmi Programu ya Kisiki Hai Mkoa wa Dodoma; Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa tarehe 19 Novemba, 2017.
Mkurugenzi wa Mradi ameeleza kwamba engo kuu la Mradi ni kuikomboa ardhi iliyochakaa ya mashamba na malisho izalishe chakula na malisho kwa wingi ili kupambana na baa la njaa na mabadiliko ya tabianchi; Aidha, Programu hii imelenga kukomboa mazingira kwa kutumia njia ya Kisiki Hai (FMNR-Farmer Managed Natural Regeneration) na njia zingine ikiwemo ya uvunaji wa maji. Awamu ya kwanza ya Programu hii inahusisha vijiji vyote vya Tarafa mbili za Kongwa na Mlali kwa Wilaya ya Kongwa, kuanzia mwezi huu wa Desemba, 2017. Pia, Programu inaunga mkono kwa 100% kampeni ya Wilaya ya Kongwa ya ONJAKO (Ondoa Njaa Kongwa) inayo ongozwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya.
Programu hii ni ya miaka kitatu (2017 hadi 2020) na itatekelezwa katika Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma ikiwa na malengo ya fuatao hadi kufikia kilele chake:
Katika Uzinduzi huu Warsha ya siku moja kwa wadau muhimu wa mazingira katika Wilaya ya Kongwa imefanyika, ambayo imehusisha viongozi wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Mashirika ya Dini, Asasi za Kiraia, Waandishi wa Habari, pamoja na Madiwani na Maafisa Watendaji wa Kata zote za Tarafa za Kongwa na Mlali. Katika warsha washiriki wamefundishwa namna ya kutumia mbinu mbalimbali katika kuendeleza visiki hai ili kuvifanya kumea vizuri na kutengeneza miti mipya na hatimaye wananchi wa Wilaya ya Kongwa waweze kupata faida zake kwa kutunza mazingira. Maazimio ya utekelezaji wa mikakati mbalimbai iliyokubaliwa imepitishwa ambapo baada ya miezi sita (6) kuanzia mwezi huu Desemba, 2017 Kongwa inatarajia kupata mabadiliko ya kijani - kwani elimu kuhusu mbinu za kuendeleza visiki hai itatolewa kwa wanachi waliopo maeneo ya mradi na wilaya nzima kwa ujumla.
Kauli mbiu ya Programu ni “KISIKI HAI-MKOMBOZI WA MAZINGIRA!”
PROGRAM YA KISIKI HAI BISH.pdf
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.