Na Stephen Jackson, Kongwa.
Rais wa shirika la Afya la kimataifa la Korea (KOFIH) Prof. Chan Yup Kim ameipongeza wilaya ya Kongwa kwa hatua nzuri ya utekelezaji miradi.
Pongezi hizo zimetolewa na kiongozi huyo Tarehe 13, Julai 2022 wakati alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kujionea hali ya utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na shirika hilo.
Kufuatia ziara hiyo, Mkurugenzi mtendaji Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo, ameeleza kuwa shirika la KOFIH limetoa sh. 230,000,000/= kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Chamkoroma pamoja na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh. 186,000,000 kwaajili ya Hospitali ya wilaya. Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mashine za usingizi na zile za kuhifadhia watoto njiti.
Miongoni mwa maeneo aliyotembelea hospitalini hapo ni pamoja na maabara, chumba cha upasuaji, na jengo la wagonjwa wa dharula.
Naye Mganga mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dkt. Thomas Samwel, amewaomba wadau wengine ikiwemo serikali kusaidia mchakato wa kupata wataalamu watakaosimamia uendeshaji wa mashine za kisasa, huku akiitaka jamii nzima kushiriki katika uboreshaji wa huduma za Afya.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Miradi wa shirika la KOFIH Dkt. Uless A. Mbise Amebainisha kuwa shirika litafanya kazi na Wilaya ya Kongwa kwa muda wa miaka mitano ikiwa huu ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji Miradi.
Prof. Chang Kim na wafuasi wake alipokelewa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na watumishi wa Halmashauri Huku burudani ya ngoma za asili ikipamba moto.
Prof. Kim na timu yake, akiwa na wenyeji wake ndani ya chumba Cha upasuaji katika hospitali ya Wilaya ya Kongwa.
Prof. Kim akitia Saini katika kitabu Cha Wageni, Hospitali ya Wilaya ya Kongwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.