Shirika la Social Action Fund (SATF) linalojihusiha na kusaidia watoto waishio kwenye mazingira hatarishi zaidi lenye makao makuu Jijini Dar es salaam kwa kushirikiana na asasi ya kidini ya FPCT Dodoma, limetoa misaada ya sare za shule na vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi 53 kwa mwaka 2025 wa shule za sekondari 8 zilizopo katika Wilaya ya Kongwa yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 12.
Stanley Mwailah Mratibu wa Asasi ya FPCT Mkoa wa Dodoma amesema lengo la kutoa misaada hiyo ni kuhakikisha watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wanafikia uwezo wa kujitegemea kwa kuwezeshwa katika maeneo ya elimu, ulinzi wa mtoto na afya Bora.
Bw. Mwailah ameeleza kuwa watoto hao waliandikishwa tangu wakiwa kidato cha kwanza na watapewa misaada hiyo hadi watakapohitimu ngazi zote za elimu kulingana na ufaulu wao na wale watakaofeli watasaidiwa kujiunga katika vyuo cha ufundi stadi (VETA).
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Kongwa, Bw. Allen Msumule amesema SATF imesaidia Sana watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuongeza kuwa maendeleo ya watoto hao shuleni ni mazuri kwani wanajitahidi kuwapa moyo wafadhili waendelee kuwasaidia ili watimize ndoto zao.
Shule za sekondari zilizosaidiwa ni pamoja na Kongwa sekondari, Sagara, chamkoroma, manghweta, sejeli, mtanana na ndaribo.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.