Na Stephen Jackson, Kongwa DC
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdalah Hamis Ulega amesema Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea na Maboresho katika Ranchi za Taifa ikiwemo NARCO KONGWA ili kutayarisha matajiri wanaotokana na Sekta ya Mifugo.
Mhe. Ulega amesema hayo Aprili 27 2023, alipotembelea Ranch ya NARCO KONGWA kwa lengo la kuzinduaa vifaa vya kisasa vya kuchakata malisho ya Mifugo.
Taarifa ya Meneja wa Ranch Bwana. Elisa Binamungu kwa waziri wa Mifugo inaeleza kuwa kiasi cha shilingi Bil. 4.65 kilitengwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya Maboresho ya Ranchi ikiwa ni pamoja na uhimilishaji wa Mifugo, kutengeneza barabara ndani ya eneo la ranchi, na kuondoa vichaka jumla ya hekta 8000 kwa ajili ya kustawisha Malisho ya Mifugo.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi wa ranchi Prof. Peter Msoffe amesema, kwa sasa ranchi imepokea ng'ombe wazalishaji 1000 ambapo kati yao majike ni 800 na madume 200 lengo likiwa ni kufikia malengo la kuongeza uuchakataji na usafirishaji wa nyama nje ya Nchi kutoka Tani elfu 17 hadi 50 nakuendelea.
Katika ziara yake Mhe. Ulega amezindua vifaa vya kisasa vya uchakataji wa malisho ya mifugo yakiwemo matrekta manne na mashine mbalimbali na hatimaye kuzungumza na wafugaji wenye vitalu katika ranchi hiyo.
Sambamba na hayo amezindua pia zoezi la uvunaji wa nyasi litakalodumu hadi Julai, 2023.
Aidha Mhe. Ulega ameridhia kujengwa Kwa kituo mahsusi cha kuuzia nyama katika eneo la njiapanda ya NARCO, Wazo lililowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani kata ya Mtanana Mhe. Joel Mussa ameshauri Serikali kuwa na mpango kazi wa kuwakopesha ng'ombe bora wananchi walio ndani na nje ya ranchi ili kuboresha hali ya mifugo.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.