Na Stephen Jackson, Kongwa.
Uongozi wa Kata ya Sagara na Kijiji Cha Ijaka Kata ya Sagara, umeishukuru Serikali Kwa kutekeleza mradi wa Maji katika Kijiji Cha Ijaka, kupitia mpango wa Maendeleo Kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya uviko 19.
Mradi huu unatekelezwa na kampuni ya FHS Engineering ambapo shughuli za ujenzi wa miundombinu zipo mbioni kukamilika na jumla ya Shilingi 78,706,234.25 zimetumika.
Kufuatia hatua hiyo, viongozi hao kwa pamoja wameuzungumzia mradi huu kama ukombozi kwa wakazi wa Kijiji Cha Ijaka, na hivyo wameiomba Serikali kukamilisha usambazaji wa miundombinu ili kuwasogezea huduma wananchi lengo likiwa ni kutimiza sera ya kumtua ndoo mama kichwani.
Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi mhandisi Alstidius Kajuna kutoka kampuni hiyo amesema kuwa utekelezaji wa Mradi huu mwanzoni ulikumbwa na Changamoto ya uwezeshwaji lakini baada ya kutatuliwa Changamoto hiyo, mradi umetekelezwa Kwa wakati na unatarajia kukamilika katikati ya mwezi Agosti, 2022
Kukamilika Kwa awamu ya kwanza ya mradi huu kutasaidia kuondoa adha ya maji Kwa wakazi wapatao 500 wa kitongoji Cha uzunguni kati ya wakazi 4259 wa Kijiji hiki.
Mradi huu ni miongoni mwa miradi inayotarajiwa kupitiwa na Mbio za Mwenge wa uhuru Agisti 23, 2022.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.