Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa imepokea shilngi millioni mianne (TSh. 400,000,000/=) kwa ajili ya kujenga majengo matano pamoja na njia ya kumbelea katika Kituo cha Afya Ugogoni.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omary Nkullo ameeleza kwamba fedha hizo zimeshaingia katika akaunti ya Halmashauri na kumtaka Afisa Manunuzi Ndugu Praygod Munisi kwa kushirikiana na Idara ya Ujenzi kuharakisha mchakato wa ujenzi wa Kituo hicho.
Aidha, Ndugu Munisi (Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi) wakati akizungunguza na Afisa TEHAMA alipokuwa akitambulisha mradi kwa wananchi wa Ugogoni, ameeleza kwamba mradi huu utahusisha ujenzi wa jengo la Upasuaji, Wodi ya Wazazi, Nyumba ya Kuhifadhia Maiti, Nyumba ya Mtumishi na Maabara. Aidha, ameelezakuwa mradi utahusisha ujenzi wa njia ya kutembelea (Walk Way).
Huu ni muendelezo wa Serikali katika mpango wake wa kuboresha huduma za afya kwa kuboresha mazingira ya vituo vya afya nchini, ambapo hapo awali Wilaya ya Kongwa ilipata kiasi cha fedha kama hiki kwa ujenzi majengo matano katika Kituo cha Afya Mlali.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.