Na Stephen Jackson, Kongwa.
Shule ya Msingi Mnyakongo Wilayani Kongwa, Mkoani Dodoma imepata misaada ya kielimu kutoka Kwa wahisani wa nchi za Uingereza na Marekani.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji (W) Dkt. Omary Nkullo muda mfupi baada ya kufanya kikao cha ndani na wahisani hao Mapema tarehe 26 Julai 2022.
Maelezo yake Dkt. Nkullo yalibainisha kuwa , wahisani hao ni wale walisomea katika Shule hiyo kipindi kampuni ya "Overseas food Corporation" ilipokuwa ikifanya kazi ya Kilimo Cha Karanga Wilayani humo.
Akizungumza Kwa niaba ya wengine, mhisani Prof. Peter Larham alisema kuwa wao wameamua kutembelea Shule waliyosoma walipokuwa watoto ili kutoa misaada kwa ajili ya kuboresha mazingira ya utoaji elimu.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mnyakongo ndugu Safari Kambadu alitaja misaada iliyotolewa kuwa ni pamoja na uchimbaji wa kisima cha maji, ujenzi wa Maktaba, vitabu, vifaa vya michezo, na ahadi ya kukarabati Shule hiyo itakayohusisha ujenzi wa uzio.
Ikumbukwe kuwa Shule hii ya kihistoria ni miongoni mwa Shule zinazofanya vizuri katika mitihani ya taifa, wilayani Kongwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.