Jumla ya madarasa manne (4), mabweni miwili (2) – yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 60 kwa kila moja, ukamilishaji wa maabala mbili (2) na matundu kumi (10) ya vyoo yanendelea kujengwa katika shule ya sekondari Ibwaga.
Utekelezaji wa mradi huu ni kuifanya shule hii kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita “High school” ambapo shule hiyo itachukua wanafunzi 120 (wasichana) kwa upande wa kidato cha tano kwa michepuo ya sayansi tu (PCB, PCM na PGM) mara baada ya kukamilika ujenzi na kukamilisha taratibu za usajili.
Ujenzi huu wa kuifanya shule ya Ibwaga kuwa “High School” ulianza Mei 5, 2017 na unatarajiwa kukamilika Juni 15, 2017 kupitia programu ya P4R.
Mradi huu unatekelezwa na mafundi wa kawaida (local fundi) kwa kutumia “force account” na unagharimu shilingi milioni 259 za kitanzania hadi kukamilika kwake.
Kukamilika kwa usajili wa shule hii kutaifanya wilaya ya Kongwa kuwa na shule mbili za sekondari zenye kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita, kwa sas ni Shule ya Sekondari Kongwa pekee ndiyo yenye wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.