Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa iko katika mchakato wa kuihamisha shule ya sekondari Kongwa. Mchakato huu unafanyika kutokana na hitaji la kubadilisha eneo iliyoka shule kwa sasa na kuwa sehemunya kihistoria, kwani eneo hilo na baadhi ya majengo yake yalitumiwa na Wapigania Uhuru wa Nchi za kusimni mwa Afrika kabla ya kuchukuliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JW) na baadaye kufanywa kuwa shule ya sekondari mwaka 1995. Kwa sasa upembuzi yakinifu wa gharama za ukarabati wa majengo kuwa kama ilivyokuwa kipindi cha kambi na kituo cha mafunzo ya kijeshi pamoja na makadilio ya ujenzi wa shule mpya kwa eneomjipya lililochaguliwa umeshafanyika. Ukarabati kambi, barabara, makaburi ya wapigania uhuru hao pamoja na ujenzi wa shule mpya utagharamiwa na UNESCO, michoro na BOQ zimeshawasilishwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa tayari kutumwa UNESCO.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.