Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kongwa Joab Ndugai April 16/2018 ameongoza mamia ya wakaziwa Kongwa na Viongozi mbalimbali Katika Ibada ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhandisi Ngusa Izengo na kusafirishwa kuelekea kwao Chato Mkoani Mwanza
kwa Mazishi.
Akitoa Salamu za Rambirambi katika viwanja vya Halmashauri ya Kongwa Ndugai alisema,Hajawahi kufanya kazi na Mkurugenzi wa aina Ya Jinsi alivyokuwa Ngusa, kutokana na umahiri wake kwa kipindi alichokuwa katika Halmashauri hiyo,Kulikuwa na Utulivu katika vikao mbalimbali Tofauti na baadhi ya wakurugenzi waliwahi kufanya kazi katika halmashauri hiyo. "Hii ni kutokana na Hekima aliyokuwa nayo Ngusa." Alisisitiza.
Pia Ndugai alisema Eneo alilopatia ajali ni eneo ambalo linatakiwa kutizamwa kwa umakini kwani ni eneo hatarishi na limekuwa likisababisha ajali Mara kwa Mara. Aidha,Padri Alanus Ngonyani wa Parokia ya Kongwa akitoa mahubiri Katika ibada ya Kuaga mwili huo akitoa mahubiri Katika ibada ya Kuaga mwili huo aliwataka wanadamu kuhakikisha wanaishi na kutenda mema katika maisha ya Kila siku ili kujiandaa na Mauti kwani ni ahadi.
Katibu wa wabunge wa Dodoma Edwin Sanda ambaye ni mbunge wa Kondoa mjini akiwasilisha Salamu za Rambirambi kwa niaba ya wabunge Mkoa wa Dodoma alisema, Ngusa alikuwa mtu aliyependa ushirikiano na watendaji wenzake kwa ujumla Wamepoteza Mtu muhimu Katika Harakati za ujenzi wa Taifa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kongwa amemshukuru mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo John Kayombo kwa namna alivyoguswa na Msiba huo na kutoa mchango wa Sanduku la Kwa ajili ya Kubebea mwili wa marehemu. "Hi inajidhihirisha ni Jinsi gani Ngusa aliishi kwa Kushirikiana na kugusa maisha ya watu" Ndejembi alieleza.
Dr.Abdulah Makame Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki akitoa salamu za Rambirambi amewapa pole wananchi wa Kongwa na kuwataka waendelee kumuombea Apumzike kwa Amani.
Kadhalika Naibu Waziri Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mh.Josephat Kakunda Katika salamu hizo alisema, Ngusa alikuwa Mbunifu, mwadilifu,mchapakazi mzalendo na mwenye uaminifu mwadilifu,mchapakazi mzalendo na mwenye uaminifu Katika utendaji wake wa Kazi na kuwataka watendaji wengine kuiga mfano huo.
Ibada Hiyo ilihudhuriwa na Viongozi Mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge, Wafanyakazi wa Halmashauri hiyo, Wakurugenzi wa Wilaya za Jirani Gairo,mpwapwa Kondoa, na wakuu wa Wilaya hizo, Madiwani wa Halmashauri hiyo pamoja na Wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali.
Ngusa alizaliwa April 14/1972 na alifariki kwa ajali katika eneo la Makaravati mpakani kwa wilaya ya Kongwa na Chamwino usiku wa April 14/2018 kwa ajali ya Gari yake Kuangukiwa na Lori la Mafuta
"Bwana Ametoa na Bwana ametwaa na Jina la Bwana na lihimidiwe"
Amen.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.