Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kongwa Dkt. Omary A. Nkullo amemkabidhi Mhe. Job Yustino Ndugai Hati ya Kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kongwa leo tarehe 30 Oktoba 2020 katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Mhe. Job Yustino Ndugai ambaye pia ni Spika wa Bunge liliopita la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amepita bila ya kupingwa katika uchaguzi wa Mkuu wa Mwaka 2020.
Uchaguzi ngazi ya Urais Mhe John Joseph Pombe Magufuli kupitia CCM ameshinda kwa kishindo kwa asilimia 97.3.
Katika ngazi ya Udiwani, madiwani wa Kata 5 – Kibaigwa, Kongwa, Mlali, Ng’humbi, na Sejeli ndiyo wamepita kwa uchaguzi na madiwani 17 katika wamepita bila kupingwa.
Aidha, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kongwa amemkabidhi hati za kuchaguliwa kwa madiwani wa Kata zote 22 za Jimbo hilo la Kongwa ambapo viti vyote vya udiwani vimechukuliwa na CCM.
Habari na Nkinde Moses
Afisa TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.