Na. Stephen Jackson, Kongwa.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Imeanzisha mpango shirikishi kwa jamii unaolenga kulinda ustawi wa miradi ya Maendeleo dhidi ya vitendo vya Rushwa Ili kuboresha Mazingira ya utolewaji wa huduma za jamii.
Programu hiyo inayojulikana Kwa kina la TAKUKURU - RAFIKI imetambulishwa na Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Kongwa Bw. Cosmas Shauri, katika mkutano wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Januari 19, 2023.
Katika mpango huo, TAKUKURU kupitia Madiwani na Watendaji wa Kata itaendesha vikao na wananchi na wadau mbalimbali waliopo ndani ya Kata husika ikihusisha uwakilishi wa Taasisi zote zilizopo katika eneo husika.
Kwa mujibu wa Kamanda Shauri, jukumu la vikao hivyo litakuwa ni kubaini na kuibua kero zinazoweza kusababisha Rushwa na kuzitafutia ufumbuzi.
Aidha wadau wanaohusika moja kwa moja na programu hii ni wananchi, watoa huduma, na mtu yeyote mwenye utayari wa kushiriki mapambano dhidi ya Rushwa.
Kufuatia mpango huo, Mbunge wa Jimbo la Kongwa na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, ameipongeza TAKUKURU kwa kuja na Mpango huo na amezishauri taasisi nyingine kuja na mipango yenye Sura ya aina hiyo.
Programu ya TAKUKURU rafiki, imelenga Sekta ya huduma za jamii zenye miradi mingi hususani Maji, Elimu, Nishati, Afya, Ardhi na miundombinu ya Barabara.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.