Bw. Ilomo ameyasema hayo katika ziara yake Wilayani Kongwa alipotembelea na kujionea mradi wa nyumba mbili za walimu zilizopo katika Kata ya Chitego Kijiji cha Chitego wilayani Kongwa ambapo amewaomba walimu pamoja na uongozi wa Kijiji kuhakikisha nyumba hizo zinatunzwa ili ziweze kuleta matarajio yaliyokusudiwa.
Aidha Bw Ilomo ameonyesha kufurahishwa na shuhuda za wanufaika wa (TASAF) hususani wanaume kutumia ruzuku walizopewa kwaajili ya kuinua uchumi wa familia na jamii zao na kubainisha kuwa kuna baadhi yao hutumia vibaya fedha hizo kwa malengo yasiyokusudiwa na mfuko na kuomba wanufaika watumie vizuri ruzuku.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Taifa kutoka idara ya ajira za muda, Mhandisi Tadei Shirima ameelezea kuwa wananchi waliopata fursa ya kupata miundombinu kama iliyojengwa Chitego ni wachache kwani ndani ya Halmashauri ya Wilaya Kongwa ni Kijiji kimoja cha Chitego hivyo anaamini kutokana na uhitaji wao watazitunza vizuri nyumba hizo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw. Fortunatus Mabula amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwatazama watanzania na kuendelea kusimamia wananchi kupata huduma muhimu, jambo linalowezesha TASAF kuwafikia wananchi na kubadili maisha yao kiuchumi. Vilevile Kaimu Mkurugenzi emeeleza Imani yake kuwa walinzi wa kwanza wa miradi ya nyumba hizo watakuwa walengwa wenyewe hivyo nyumba hizo zimekabidhiwa kwa watu sahihi watakaotunza miundo mbinu hiyo.
Nae mratibu wa TASAF mkoa wa Dodoma Bi. Josephine Pascal amewataka walengwa kutambua fedha zinazotolewa na TASAF ni za Serikali ya awamu ya sita na ni juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, fedha ambazo zinatolewa kwaajili ya kuwakwamua wananchi dhidi ya umasikini.
Vilevile Diwani wa Kata ya Chitego Mhe. Peter Kalunju ameomba uongozi wa TASAF kujenga mabweni katika shule ya Chitego ili kuwasaidia wanafunzi wanaotembea umbali mrefu kufika shuleni kwa uharaka ili kupata muda wa kutosha wa kujisomea katika mazingira ya shule.
Pamoja na hayo wakitoa shuhuda zao walengwa wa TASAF wilayani Kongwa wamesema kuwa fedha wanazopata zimewasaidia kuinua uchumi wa familia zao kwa kufanya mambo mbalimbali kama kujenga nyumba za bati, kusomesha watoto, kununua mifugo, kununua mashamba na chakula na kutoa shukrani zao za dhati kwa uongozi mzima wa TASAF Pamoja na Serikali ya awamu ya Sita.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.