Timu ya CHF (Mfuko wa Afya ya Jamii) ya Wilaya ya Kongwa imejipanga kufanya uhamasishaji wa wengi (Mass Sensitization) ili kuvutia wanachama wengi kujiunga na Bima ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Mejana wa CHF, Daktari Francis Lutalala akiongea na Afisa TEHAMA (W), Ndugu Nkinde Moses ameeleza kuwa uhamasishaji huu unaanza rasmi tarehe 11 Agosti 2017 na zoezi hili litakuwa endelevu hadi kufikia mwezi Desemaba 2017. Lengo kubwa ni kufikia uandikishaji wa asilimia hamsini (50%) au zaidi ya kaya zilizopo wilayani Kongwa.
Aidha, ameeleza kwamba, zoezi hili litaneda sambamba na uhuishaji wa wanachama wa zamani, kuondoa changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwa wanachama pamoja na kueleza mpamngo mpya wa Serikali wa kuboresha huduma za Afya kupitia CHF iliyoboreshwa. Katika uhamasishaji huu, majibu ya kero/maswali yote waliyonayo wananchi kuhusu suala la CHF yatajibiwa.Ratiba ya Mikutano kijiji kwa kijiji itatolewa tarehe 10 Agosti, 2017 pamoja na barua kwa viongozi wa vijiji kuhusu maandalizi ya mikutano na wananchi.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.