Timu ya wanamichezo watumishi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa imefanya ziara ya michezo ya kirafiki Wilayani Manyoni, Mkoani Singida na kurejea salama.
Ziara hii imeanza tarehe 28 Agosti na kukamilika leo tarehe 29 Agosti, 2021 ambapo ikiwa Wilayani Manyoni imeshiriki michezo 3 ya kirafiki na kupoteza michezo yote. Katika mchezo wa mpira wa miguu timu ya Manyoni iliibuka na ushindi wa goli 2 kwa 1. Kwa upande wa mchezo wa wavu, timu ya Manyoni imepata seti 2 na Kongwa seti 1 na katika mpira wa pete timu ya Manyoni pia iliibuka kidedea kwa goli 11 kwa 8.
Afisa Michezo wa Wilaya ya Kongwa, Bw. Kelvin Msumule ameeleza kwamba sababu ya timu za Wilaya yake kupoteza michezo hii ni kutokana na timu kusimima kwa muda mrefu bila ya kufanya mazoezi ya pamoja wakati wa shughuli za maandalizi ya Mbio za Mwenge 2021 na janga la Uviko 19. Hata hivyo, amesema kwamba sasa wamejipanga na wanarudi upya, hivyo timu yeyote itakayopita mbele yao ijiangalie sana na sasa wanajipanga kufanya ziara Wilayani Karatu, Arusha na Mkoani Morogoro.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.