Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe.George Simbachawene amezitaka Sekretarietiza Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwawezesha Maafisa Habari waliopochini ya Ofisi zao kutekeleza majukumu yao kwa wakati na haraka ili kuendana nakasi ya ukuaji wa kiteknolojia na kupashana habari ili kuwaletea Wananchimaendeleo.
Mheshimiwa Simbachawene ameyasema hayo mjini Dodoma, wakati akizindua tovuti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazozitatumika katika uwasilishaji wa habari na taarifa muhimu kwa Wananchi.
"Nawaagiza Wakuu wa Mikoa wote kuhakikisha Maafisa Habari katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wanawanunulia vifaa hivi muhimu kama kamera, mtandao wa kompyuta, kompyuta na vinginevyo vya kufanyiakazi hizi muhimu ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa na kwa gharama ya ofisi ili waweze kuwapatia Wananchi taarifa, ikiwa ni haki yao ya msingi ya kupatataarifa," alisema Mhe.Simbachawene.
Mhe.George Simbachawene amesema, kwa kuwa Tanzania iliweka saini Azimio la 'Open Government Partnership' mwaka 2011, kuweka uwazi wa shughuli za Serikali kwa Wananchi, ikiwa na lengo la kuimarisha Utawala Bora, kuondoa rushwa na kujenga imani kwa Wananchi wake na Azimio linaweka msisitizo kwa Wananchi kupata taarifa kwa wakati na uhuru zaidi.
Aidha, Mhe.Simbachawene amewataka Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha kwamba tovuti zao zinakuwa na taarifasahihi na za kutosha na zinatolewa kwa wakati.
Pia, amewataka Watendaji katika Mikoa na mamlakaza Serikali za Mitaa kuondoa urasimu katika kutoa taarifa. "Lazima taarifa zitolewe kwa wakati ili tovuti hizi zitumike kweli kwa malengo yaliyokusudiwa," alisisitiza Mheshimiwa Simbachawene.
Waziri Simbachawene aliwashukuru Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani USAID kwa kuwezesha Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ambao kupitia ufadhili huo umeweza kuendesha mafunzo ya utengenezaji wa tovuti hizo.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Sanaa,Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe aliwataka Maafisa Habari kutowaangusha Wananchi katika kuwapa taarifa pasipo urasimu wowote.
Waziri Mwakyembe amewataka Maafisa Habari kuhakikisha kuwa tovuti hizo zisigeuke kuwa magofu ya habari bali majokofu kwa kupata habari mpya kila siku.
Katika mafunzo hayo, Maafisa habari, na MaafisaTehama kutoka Halmashauri 185 na Mikoa 26 walishiriki Mafunzo hayo na kufundishwa namna ya kuandaa taarifa mbalimbali katika tovuti zao.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.