Na Stephen Jackson, Kongwa.
Maafisa Watendaji wa Vijiji na kata wametakiwa kutoa ushirikiano Kwa vikundi na wajasiriamali wanaonufaika na mikopo ya 10% kutoka Halmashauri ili kuwajengea uwezo wa kurejesha mikopo hiyo.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kongwa Bibi Paskalina Duwe Siku ya Jumatano Agosti 10, 2022 wakati alipotelea shamba la Mkulima Sendea Johnas Mnyanduli ambaye anaendesha mradi wa kilimo Cha umwagiliaji kwa mkopo wa Shilingi 6,700,000/=.
Akizungumza shambani hapo mjasiriamali Mnyanduli, alitaja Changamoto zinazokabiri mradi wake, ikiwa ni pamoja na kupanda Kwa bei za Mafuta.
Naye Afisa ugani wa kata hiyo Ndugu Philemon Kibona ameitaka Serikali kuendelea kuwezesha utatuzi wa Changamoto mbalimbali ikiwemo za usafiri ili kuwawezesha maafisa ugani kuwafikia Wakulima.
Kufuatia hatua hiyo Viongozi wa Kijiji na kata ya Matongoro, wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kama sehemu ya kufanikisha jitihada za Serikali.
Ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo kupitia mikopo ya asilimia kumi ilihusisha timu ya wataalamu wa Maendeleo ya jamii ilivyokuwa ikiwa ikiwajengea uwezo vikundi kujisajili kwenye mfumo mpya wa kusajili vikundi unaojulikana kama TPLMIS.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.