oezi la kula kiapo Cha uadilifu na kutunza Siri kwa viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba limefanyika katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kongwa.
Katika zoezi hilo, viongozi hao ambao ni pamoja na walioshinda nafasi za Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Kitongoji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji kundi mchanganyiko pamoja na kundi la wanawake wameaswa kuishi viapo vyao pamoja na kuhakikisha wanakuwa waadilifu na kutotumia nyadhfa zao kujinufaisha bali wazitumie kwa maslahi mapana ya kuwatumikia wananchi pamoja na kutatua kero zao.
Kwa upande wao viongozi mbalimbali wameonyesha ari ya kuwatumikia wananchi pamoja na shauku ya kuanza majukumu Yao Ili kutimiza ahadi walizowaahidi wananchi kipindi walipokuwa wanaomba Kura.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.