Wanufaika wa mikopo ya vikundi inayotolewa na Halmashauri kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii wilayani Kongwa, Wameiomba Serikali kuwakopesha Zana za Kilimo hasa Matrekta na Mashine za kuchakata Mafuta ya Alizeti ili waweze kujikwamua Kiuchumi.
Ombi hilo limetolewa na Wanakikundi wa vikundi vya Tunaweza na Msembe kutoka kata ya Ngomai vinavyojishughulisha na kununua, kukamua na kuuza mafuta ya Alizeti, wakati wa ziara ya Maafisa Maendeleo ya jamii wilaya inayoendelea kwa lengo la kukagua Miradi ya vikundi vilivyopewa Mikopo hiyo.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Tunaweza Bibi Perisi Mazengo, ameeleza kuwa mikopo hiyo licha ya kuwasaidia kuondokana na riba kubwa walizokuwa wakitozwa na matajiri, pia imewasaidia kusomesha watoto wao.
Afisa Mikopo Idara ya Maendeleo ya Jamii wilayani Kongwa Bwana Joseph Mshana, Amewasisitiza wanakikundi wa vikundi hivyo kuzingatia kanuni na taratibu za biashara ya Mafuta ya Alizeti ikiwa ni pamoja na kushirikisha wataalamu wa afya na pia Uwekaji wa lebo katika bidhaa zao ili kuongeza tija ya Mikopo hiyo.
Naye afisa Maendeleo, Bwana Alen Msumule, ameongeza kuwa, umefika wakati ambapo vikundi havitatakiwa kuzidi watu kumi ili mikopo hiyo iweze kuwanufaisha.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.