Wajumbe wa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT) ya Kongwa wapewa mafunzo ya Kiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo Elekezi ya Awali kwa Watumishi Wapya wa Sekretariati za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM). Mafunzo haya yameendeshwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji Mifumo katika Sekta za Umma (PS3) ambao ndiyo walioandaa kiongozi (manual) kitakachotumiwa na waajiri katika kutoa mafunzo elekezi ya awali kwa waajiriwa wapya.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kongwa, Mhandisi Ngusa L. Izengo. Mwezeshaji ameeleza kuwa lengo kuu la Kiongozo cha Mafunzo Elekezi ni; Kufafanua umuhimu wa mafunzo elekezi kwa waaajiriwa wapya, Kuainisha wadau mbalimbali na majukumu yao katika utekelezaji wa mafunzo elekezi( mafunzo ya awali ya uelewa wa mazingira ya kazi -Orientation na uelewa wa kazi - Induction), Kuweka mfumo au utaratibu unaofanana wa kutoa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya, Kuwakumbusha waajiri kuhusu matakwa ya Sera, Kanuni, Nyaraka na Miongozo ya mafunzo elekezi katuka Utumishi wa Umma.
Mafunzo haya yalihitimishwa kwa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT) kuandaa mpango wa utekelezaji kuanzia robo hii ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018, ambapo mikakati mbalimbali imewekwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.