Serikali kupitia Wakala wa Vipimo Tanzania Bara, inaendelea kuwasisitiza Wakulima na Wafanyabiashara wa mazao kuepuka ufungashaji wa lumbesa na kutumia vipimo halali kutokana na madhara Mengi yatokanayo na ufungashaji huo pamoja na kuhakikisha wanatumia mizani ambayo haijaharibika.
Afisa wa Wakala wa Vipimo Tanzania Bara, Mkoa wa Dodoma Bw. Saidi Ibrahim June 27, 2018 amewaeleza Wajumbe wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Kongwa kuwa kazi kubwa inayofanywa na Taasisi ya Wakala wa Vipimo Tanzania ni kusimamia matumizi sahihi ya Vipimo vya aina zote ili ikiwemo vipimo vya ujazo, uzito na urefu na kupiga marufuku Vipimo batili, yaani visivyo na ulinganifu.
Bw. Ibrahim amesema ufungashaji wa Lumbesa ni Ukiukwaji wa Taratibu za Vipimo na ameyataja madhara ya Lumbesa ni pamoja na kumpunja mkulima kutokana na ujazo huo kuzidi ujazo wa gunia la kawaida, hivyo mkulima hulazimika kuuza Lumbesa kwa bei ya ujazo wa kawaida.
Madhara mengine ni ya Kiafya kwa wabebaji, kutumia nguvu nyingi kupita uwezo wao na kutokuwa na uwiano kati ya Kilo za mbebaji na mizigo iliyofungashwa kwa mfumo huo wa Lumbesa, pia, huharibu miundombinu na kuharibu vyombo vya usafiri.
“Aidha, Lumbesa hudhoofisha ukusanyaji wa mapato, kwani mwenye mazao anapotozwa tozo kwa gunia moja huku amefungasha lumbesa ni dhahiri ufungashaji wa Lumbesa hupita vipimo halisia”. Amesisitiza Bw. Ibrahim.
Dinah Mlay ni mmoja wa Wafanyabiashara watumiao mizani ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Biashara kupitia Sekta Binafsi amesema, “kumekuwa na Changamoto za gharama kubwa za mafundi warekebisha mizani ambapo gharama hizo huzidi gharama ya manunuzi ya mzani mpya, hivyo anaomba Taasisi hiyo kuliangalia suala hilo kwa undani”. Aidha, Ibrahim alisema Faida ya Vipimo halisia vinakuza uchumi binafsi na uchumi wa Taifa, na kusaidia katika soko la ushindani ndani na nje ya nchi.
Ambapo Bw. Ibrahim amesema amelipokea na sehemu husika. Aidha,Sheria ya Vipimo inataka Vipimo vyote ikiwemo mizani, pampu za mafuta kukaguliwa na maafisa vipimo Mara moja kwa kila mwaka. Hivyo, Mlaji asipofanya hivyo, atakuwa amevunja sheria ya Vipimo
Pia, Bw. Ibrahim amesema Faida ya Vipimo halisia vinakuza uchumi binafsi na uchumi wa Taifa, na kusaidia katika soko la ushindani ndani na nje ya nchi.
Mwishowe, Wajumbe wa Baraza wakapata mafunzo ya Vitu muhimu vya kuzingatia katika Ufungashaji wa mvuto wa bidhaa mbalimbali, ambapo Bw. Ibrahim alibainisha kuwa ni kuhakikisha Bidhaa inakuwa na Jina, mahali inapotengenezwa, Jina la msambazaji, Anuani ya Posta, Barua pepe, Simu, Kiasi halisi cha Vipimo cha bidhaa, lugha inayotafsirika mahali inapoenda kuuzwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.