“Tatizo la viwavi jeshi vamizi kama halitoshughulikiwa haraka na kwa pamoja litaathiri mashamba ya watu wengi. Ninawaomba viongozi wa Kata na Wataalam kuitisha mikutano na kutualika maafisa kilimo ili tuweze kutoa mafunzo na maelekezo ya namna ya kukabiliana na viwavi hawa”…amesema
Afisa Kilimo, Ndugu Elias Chilemu wakati akiongea na baadhi ya wakulima wa Kata ya Hogoro.
Aidha, Ndugu Elias Chilemu (wa pili kutoka kushoto katika picha) amewaomba wataalam na viongozi wa kisiasa kushirikiana kwa pamoja (kupitia mikutano ya hadhara) kuhakikisha elimu ya kupambana na kudhibiti viwavi jeshi vamizi inatolewa kwa bidii kwa wakulima wote Wilayani Kongwa.
Baadhi ya wakulima walipohojiwa walionesha kutowafahamu viwavi hao waliowalinganisha na aina nyingine ya viwavi wanaojulikana kwa jina la asili “SULENJE”.
Pamoja na changamoto hiyo iliyobainika, wakulima hao wamehimizwa kujenga mazoea ya kukagua mashamba yao mara kwa mara ili viwavi hao wanapojitokeza waweze kudhibitiwa mapema.
Aidha amewaelekeza madawa ya kutumia pamoja na sehemu yanapopatikana.
“Madawa ya kukabiliana na wadudu hawa waharibifu yanapatikana kwenye maduka mengi
ya pembejeo za kilimo, hivyo naomba wakulima myanunue na kunyunyiza kwenye mimea mapema kabla ya shambulio la wadudu hawa kujitokeza wakati jitihada za Serikali zinaendelea kufanyika”…alisema Chilemu.
Viwavi Jeshi Vamizi hushambulia sana mimea aina ya mahindi na mtama.
Chanzo : Godfrey Mville (Kaimu Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa)
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.