Wanafunzi wa chuo kikuu cha St John's Dodoma wametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na kufanya usafi wa mazingira Pamoja na kutoa msaada wa mashuka 50, sabuni, maji, na viburudisho kama biskuti na juisi vyenye thamani ya shilingi milioni 1,426,000 katika hospital ya Wilaya ya Kongwa.
Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wa chuo cha St John’s Rais wa Chuo, Bwana Ivo Livingstone Augustino amesema kuwa lengo lao kubwa ni kuhudumia jamii inayowazunguka kwa upendo na kudumisha ushirikiano.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Afisa Tarafa ya Zoissa Bwana Denis Mbawi ameshukuru uongozi wa chuo cha St John's kwa mchango walioutoa kwa jamii kwa kuyakumbuka makundi yenye mahitaji wakiwemo wagonjwa na kwamba huu ni mfano bora wa kuigwa na makundi mengine katika jamii.
Akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Mganga mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dkt Thomas Mchomvu baada ya kushukuru, pia amewataka wanafunzi hao kwenda kutangaza mambo mazuri yaliyopo katika Wilaya ya Kongwa na kuwafanya watu wengine wavutiwe zaidi kutembelea.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.