Na Stephen Jackson, Kongwa DC
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka, ametoa wito kwa wanafunzi wenye vipaji mbalimbali vya sanaa na michezo kuchangamkia fursa mbalimbali ili kukuza vipaji vyao.
Akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari Manghweta iliyopo Kata ya Chamkoroma Tarafa ya Mlali, Mhe. Mayeka alisema, licha ya kushiriki shughuli za michezo wanafunzi wanapaswa kuzingatia masomo yao ili kujijengea mstakabali wa maisha yao.
Katika hotuba yake, DC Mayeka aliwasisitiza walimu kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi kukuza vipaji vyao vya sanaa na michezo, huku akionya tabia ya baadhi ya Wanafunzi kuacha masomo pindi wanapoanza kuonja matunda ya vipaji vyao. "kuna wengine wakishalewa umaarufu kidogo, wanaacha na Shule" alinukuliwa Mayeka.
Mayeka alisema hayo wakati Kamati ya usalama ilipotembelea shule hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi na maeneo ambayo mbio za mwenge, wa uhuru zitapita, manamo mwezi Juni 2024.
Aidha Mhe. Mayeka amewaahidi Wanafunzi hao kuwapatia Mpira, pindi atakapotembelea shule hiyo kwa awamu nyingine, kauli ambayo wanafunzi wameipongeza.
Ziara hiyo ya Kamati ya usalama na wataalamu imetembelea na kukagua maeneo na miradi mbalimbali katika Tarafa za Mlali na Kongwa ikianzia Kata ya Chamkoroma na kuhitimisha Kata ya Sejeli, eneo lililopangwa kwa ajili ya Mkesha wa Mwenge.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.