Na Stephen Jackson, Kongwa DC
Kufuatia tahadhari iliyotolewa hivi karibuni na Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA), kuhusu uwezekano wa kunyesha mvua kubwa za Elnino, Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari Ili kukabiliana na hali hiyo.
Akiwa katika ziara Maalumu Wilayani Kongwa, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bwana Ally Gugu Oktoba 26, 2023, amewataka viongozi Wilayani hapa kutoa Elimu Kwa Wananchi Ili waweze kujiandaa kukabiliana na mvua za elnino ambazo zimetabiriwa kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
"Ndugu zangu kama tunavyoendelea kuhimizwa na mamlaka ya hali ya hewa, tunatarajia kuwa na mvua nyingi mwaka huu kwa hiyo niendelee kusisitiza tuchukue tahadhari kwa kuweka mazingira wezeshi kwa kipindi hicho ili kujiepusha na athari zake " Gugu alisema wakati akizungumza na wakuu wa Divisheni na Vitengo Wilayani Kongwa.
Kwa upande wake Dkt. Omary A. Nkullo, Mkurugenzi Mtendaji (W) aliahidi usimamizi uliotukuka katika utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi na kwamba dhamira yake ni kutoangusha jitihada za Serikali.
Katika ziara yake Katibu Tawala Mkoa Bwana Gugu, alitembelea baadhi ya miradi ya Maendeleo inayotekelezwa Wilayani Kongwa ukiwemo mradi wa Shule ya mpya ya Sekondari Manungu kupitia (SEQUIP) ambayo imekamilika kwa 95%, Nyumba ya Mkurugenzi ambayo ujenzi wake umekamilika na Jengo jipya la Halmashauri ambalo ujenzi wake upo nyuma Kwa siku 81 na umefikia 41%..
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.