Na Stephen Jackson, Kongwa
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka, amewataka wananchi Wilayani Kongwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu kwa kuzingatia kanuni zote za usafi wa mazingira na maandalizi ya chakula.
Mayeka alitoa tahadhari hiyo wakati akihitimisha kikao Cha Kamati ya Afya ya Msingi (PHC) kilichofanyika ukumbi wa Hospitali ya Wilaya Februari 14, 2024 kufuatia taarifa ya dharura iliyowasilishwa na Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Dkt. Thomas Ndalio Samwel, iliyodokeza kuwepo kwa mlipuko wa kipindupindu ndani ya mkoa wa Dodoma.
Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni pamoja na Mpango wa utoaji chanjo ya ugonjwa wa surua na rubella kwa watoto, ambapo jumla ya watoto 83,000 Wilayani Kongwa, wanatarajiwa kuchanjwa kupitia kampeni maalum inayoendelea kuanzia tarehe 15 Februari, 2024.
Akiwasilisha taatifa ya utoaji chanjo ya Surua na Rubella, mratibu wa chanjo - DIVO (W) Ndugu Cosmas Mlimila alifafanua chanzo, madhara na jinsi ya kupambana na ugonjwa huo hatari kwa watoto na jamii kwa ujumla..
Kufuatia kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi (W) ya Kongwa Bwana Fortunatus Mabula - Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu amechukua hatua za makusudi za kuhakikisha jamii inahamasishwa kuchukua tahadhari dhidi ya mlipuko wa kipindupindu na na kushiriki kampeni ya chanjo ya Surua na Rubella.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.