Na Stephen Jackson, Kongwa.
Mratibu wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Mkoa wa Dodoma, Dkt. Missana Yango amewataka wananchi kupuuza upotoshaji unaofanywa na watu mbalimbali Kuhusu chanjo ya UVIKO 19.
Dkt. Yango amesema hayo wakati wa ziara ya uhamasishaji chanjo tarehe 08 Julai, 2022 kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ofisi ya Kata ya Nghumbi alipokutana na viongozi wa kata, vijiji na vitongoji.
Kauli hiyo ilikuja baada ya wananchi kubainisha vikwazo vinavyoathiri kampeni ya utoaji chanjo ya UVIKO 19 kuwa ni pamoja na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu maarufu pamoja na kutafsiriwa vibaya Kwa dhana ya kuchanja kwa hiari.
Kwa Mujibu wa Mratibu wa Chanjo (W), kwa wastani watu 4,000 wilayani pote hupatiwa chanjo kila siku, tangu kuanza kwa kampeni ya siku kumi inayotarajia kudumu hadi tarehe 15 Julai, 2022.
Dkt. Yango alifuatana na Mratibu wa chanjo (W) ndugu Cosmas Mlimira na wataalamu wengine.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.