Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Sitaki Senyamule amewataka wananchi kudumisha amani kwa kushiriki katika masuala ya ulinzi na usalama wao.
Mhe. Senyamule amesema ukosefu wa amani unarudisha nyuma maendeleo ya wananchi hivyo ni jukumu la kila Mwananchi kushiriki katika ulinzi wa amani na kuhakikisha wizi na uporaji hasa wa pikipiki unakomeshwa.
Kupitia rai hiyo, mhe. Senyamule ameliagiza Jeshi la polisi Wilayani Kongwa kuimarisha ulinzi ikiwemo kijiji cha Mlali.
Mhe. Senyamule amesema hayo katika mkutano wa hadhara wakati akihutubia wananchi wa Kijiji cha Mlali wakati wa ziara yake ya kikazi ya Siku moja Wilayani Kongwa.
Amewataka wananchi kwa pamoja kumuombea Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa dhamira zake za dhati za kuwaletea wananchi Maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel amewataka wananchi kuacha chuki kwa viongozi wanapopiga vita uharibifu wa Mazingira kwani yeye yupo tayari kuchukiwa Ili kunusuru Mazingira.
Akiwa Mjini Kibaigwa, Mhe. Senyamule amekagua Barabara mpya ya lami inayoingia katika soko la mahindi la Kimataifa, ambapo amewaasa watumiaji wa barabara zilizopo mjini hapo kuzitumia kwa nidhamu na kwa kuzingatia maelekezo ya mamlaka husika.
Sambamba na hayo Mhe. Senyamule amesikiliza kero Mbalimbali kutoka kwa wananchi ambapo wataalamu kutoka Halmashauri na taasisi za umma Wilayani Kongwa walipata fursa ya Kujibu.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Senyamule imehitimishwa kwa kutembelea na kukagua ujenzi wa Kituo mahiri cha kudhibiti Sumu kuvu katika eneo la Mtanana kinachojengwa kwa thamani ya takribani shilingi bilioni kumi na tisa (19), ambapo ameridhishwa na hatua za ujenzi wa Kituo hicho.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.