Na Stephen Jackson, Kongwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel, amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika zoezi la Anwani za Makazi na Postikodi linalotarajia kuanza hivi karibuni wilayani hapa.
Mhe. Emmanuel ametoa wito huo wakati akihutubia mkutano wa wananchi wa Mji mdogo wa Kibaigwa waliojitokeza katika Hafla fupi ya uzinduzi wa zoezi Hilo Februari 28, 2022.
Katika hotuba yake, Mhe. Mkuu wa Wilaya amewataka Wananchi kutunza vibao vya anwani za Makazi na kulinda Miundombinu yote itakayowekwa wakati wa utekalezaji wa zoezi hilo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dr. Omary Nkullo, ametoa Rai kwa Wananchi wa Mji wa kibaigwa kujitokeza kutuma Maombi ya kazi kwa kuzingatia Tangazo lililotolewa ambapo mwisho wa kupokelewa kwa maombi ni Tarehe 2 Machi, 2022 Saa 9:30 Alasiri.
Ndugu Adam Mwenda mkazi wa kitongoji cha Mpakani, Kibaigwa, ameeleza kuwa zoezi hilo litarahisisha mawasiliano, baina ya wananchi ingawa ametaja changamoto ya Barbara na maeneo mengi kutorasimishwa, Jambo linaloweza kukwamisha zoezi hilo.
Uzinduzi wa Anwani za Makazi ngazi ya Wilaya umefanyika katika Makutano ya barabara ya Morogoro na soko la Kibaigwa ambapo Mkuu wa Wilaya Mhe. Remidius Emmanuel alikata utepe katika kibao kipya cha anwani ya barabara hizo kuashiria kuanza kwa zoezi Hilo.
Hafla hiyo ya Uzinduzi wa Anwani za Makazi iliyoratibiwa na kamati maalumu inayoundwa na wataalamu 12 kutoka Halmashauri, ni mwendelezo wa hatua za kujenga uelewa kwa Wananchi wilayani humo ili kufikia Malengo ya zoezi hilo.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.