Na Stephen Jackson, Kongwa.
Mkuu wa Idara ya Maedeleo ya Jamii Wilaya ya Kongwa Bibi Paskalina Duwe amewataka wanufaika wa Mikopo ya vikundi inayotolewa na Halmashari kupitia Idara hiyo, kuzitumia vizuri Fedha hizo ili waweze kutimiza Malengo waliyoombea mikopo hiyo.
Bibi Paskalina Duwe aliyasema hayo Tarehe 14 Disemba, 2021 wakati alipokuwa akihitimisha Mafunzo ya Kuwajengea uwezo wanawake vijana na walemavu kutoka vikundi mbalimbali walioomba Mikopo hiyo Wilayani Kongwa.
Katika Maelekezo yake aliwataka wananufaika hao kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi mbalimbali watakaohitaji kupata mrejesho kuhusu Matumizi ya Mikopo hiyo.
Katika mafunzo hayo, Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani lilitolea ufafanuzi juu ya utaratibu wa kisheria kuhusu Matumizi ya vyombo vya moto ikiwemo pikipiki zilizotolewa kupitia mikopo hiyo.
Akiwasilisha Mada katika Mkutano huo, Mkaguzi wa jeshi la polisi kutoka kitengo cha Usalama Barabarani wilayani Kongwa, aliwataka wanufaika wa mikopo ya pikipiki kuzingatia taratibu, sheria na kanuni za usalama barabarani, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha madereva wote wanakuwa na leseni.
Aliongeza kuwa kupitia umoja huo jeshi la Polisi Wilayani kongwa kwa kushirikiana na vikundi hivyo wataalika wataalamu wa mafunzo ya udereva kuwafundisha na hatimaye kuwapatia vyeti madereva watakaofudhu ili viwasaidie kupata leseni.
Mikopo hiyo inatokana na Asilimia 10% ya Mapato ya ndani kwa Kipindi cha robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2021/2022.
Katika Hafla hiyo Kila kikundi kilijaza mkataba wa makabidhiano ya Fedha baina yake na Halmashauri pamoja na michanganuo ya marejesho.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.