Na Bernadetha Mwakilabi
Habari - Kongwa DC
Wasimamizi 44 wa Uchaguzi ngazi ya Kata katika Jimbo la Kongwa wamekula kiapo cha kujitoa uanachama au kutojihusisha na chama chochote cha Siasa katika kipindi cha uchaguzi pamoja na kiapo cha kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Ya Kongwa Bi Sara Mwalilino.
Akiongea wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi hao wa uchaguzi ngazi ya Kata msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la kongwa Bw. Deodatus Mutalemwa amewasisitiza wasimamizi kuzingatia mambo mbalimbali ikiwemo kusoma kwa makini na mara kwa mara Katiba, sheria, kanuni, taratibu, na miongozo inayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi na kutolea taarifa suala wasilolielewa.
Nae Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kongwa Bi. Mwalilino wakati akiwaapisha wasimamizi hao amewataka kutenda haki katika kazi wanayokwenda kuifanya kwa kuwa inahitaji uadilifu na usiri wa hali ya juu.
Wasimamizi hao wamekula kiapo hicho mapema leo kabla ya kuanza kwa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Kata yanayofanyika Wilayani Kongwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.