Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na baadhi ya watumishi walio chini ya Idara na Vitengo wapatiwa mafunzo ya uandaaji wa Mpango Mkakati (SP).
Kwa mujibu wa Afisa Mipango wa Wilaya, Mafunzo haya yana lengo la kuandaa mpango mkakati mpya wa Halamashauri kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Mafunzo haya bado yanaendelea katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Uchunguzi wa Trakoma (KTP) uliopo Kongwa Mjini na yanatarajia kumalizika Ijumaa tarehe 30 Juni, 2017.
Baada ya mafunzo haya, kila Idara na Kitengo vyote vilivyopo Halmashauri vitatoka na SP yake ambayo itakuja kuunda SP ya Halmashauri baadaya ya kuwashikirisha wadau mbalimbali kupitia mikutano na vikao vya Halmashauri.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.