Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa inatarajia kutoa bure vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wadogo walio chini ya miaka mitano (5) Wilaya nzima.
Zoezi hili linatarajiwa kuanza rasmi tarehe 15 Machi, 2019 ambayo ni siku ya uzinduzi wa kampeni hiyo; Kampeni hii itaendelea hadi tarehe 28 Machi 2019. Aidha, zoezi la utoaji vyeti kwa watoto walio chini ya miaka mitano kwa sasa litakuwa chini ya Halmashauri.
Kampeni hii ya Utoaji wa vyeti kwa watoto wote walio chini ya umri wa miaka mitano umedhaminiwa na UNICEF na Serikali inatekeleza Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA); ambapo kwa sasa mradi unatekelezwa katika wilaya zote za mikoa ya Dodoma na Singida na tayari limeshafanyika katika mikoa 11.
Kwa watoto wote walio na miaka mitano au zaidi pamoja na watu wazima ambao hawana vyeti vya kuzaliwa wanatakiwa kufika Ofisi za Mkuu wa Wilaya au RITA na watahitajika kulipia.
Kauli mbiu ya Kampeni hii ni "Mtoto anastahili cheti cha Kuzaliwa, Mpe haki yake"
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa anawakaribisha wananchi wote kujitokeza katika zoezi hili. Hii ni fursa kwa wananchi wote ambao watoto wao walio chini ya umri wa miaka mitano hawana vyeti.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya
Anuani ya Posta: S.L.P 57 Kongwa, Dodoma
Simu ya Mezani: +255 26 2370031
Simu ya Mkononi: +255 713399349
Barua pepe : ded@kongwadc.go.tz
Copyright ©2022 Kongwa District Council . All rights reserved.